Joy FM
Joy FM
10 March 2025, 13:43

Serikali na mashirika yanayohudumia wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamewataka vijana kuachana na makundi yanayoweza kuwaingiza katika kufanya vitendo viovu ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani ndani ya kambi na nje.
Na Tryphone Odace
Vijana wanaoishi katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wametakiwa kutokubali kutumiwa na makundi yenye nia mbaya Kwa ajili ya uvunjifu wa Amani ndani ya kambi na nje ya kambi hiyo kwani kufanya hivyo watasababisha kutokuwa na Amani katika maeneo ya yao na hata nchi wanapotokea.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa huduma za wakimbizi kutoka wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania Sudi Mwakibasi wakati akizungumza wakimbizi waishio katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu Mkoani Kigoma

Amesema baadhi ya vijana wamekuwa wakitumika vibaya na watu wenye nia mbaya Kwa lengo la kuvuruga Amani iliyopo hivyo kusababisha vitendo vya mauwaji na ukatili kuendelea kuwepo.
Hata hivyo Mwakibasi amewataka viongozi wa kidini kuendelea kuhubiri Amani makanisani na kutoa elimu ya usalama kwa vijana na kuwasihi kuacha vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji na wauwaji.
Naye Afisa mwandamizi kitengo cha GBV kutoka UNHCR Rehema Gatega amesema kuwa kuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha hakuna vitendo vibaya vinavyoweza kuwakabili wakimbizi wote wanaoishimkatika kambi hiyo.
Baadhi ya wakimbizi kutoka kambi ya Nyarugusu hasa wanawake wameomba Serikali na mashirika ya kuhudumia wakimbizi kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na vitendo viovu wanavyokutana navyo ikiwemo ubakaji hasa wanapoenda kutafuta kuni.
