Joy FM
Joy FM
7 March 2025, 14:40

Mawakala wa mabasi wanaofanya shughuli zao katika mkoa wa Kigoma na Tabora wanaofanya shughuli za usafirishaji wameaswa kuzingatia kanuni za ushafirishaji.
Na Orisa Sayon
Chama cha Mawakala wa mabasi Kigoma na Tabora (KITA) kwa kushirikiana na Jumuiya ya wacongomani waishio mkoni kigoma nchini Tanzania kimezindua mradi wa pamoja wa shughuli za usafirishaji kwa nchi hizo mbili Tanzania na Congo.
Mradi huo umezinduliwa kati ya chama cha mawakala na wapiga debe wa Kigoma na Tabora (KITA) SOZA Company Limited kugundua changamoto zinazokumba za shughuli za usafirishaji kati ya kongo na Tanzania hasa mkoani Kigoma.
Patrick Pius ni mwanachama wa chama cha mawakala wa mabasi Kigoma na Tabora ( KITA)/SOZA Compani Ltd na miongoni mwa malengo ya kuzindua mradi wa umoja huo ni pamoja kutatua changamoto ya utapeli katika shughuli hizo huku Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wakongomani wai Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wakongo Mch, Dunia David shio Kigoma(CCT) Mch, Dunia David akieleza changamoto wanazokumbana nazo wasafirishaji kutoka nchini Kongo.
Mkurugenzi Mtendaji wa SOZA Company Ltd inayojishughulisha na kufanya utafiti kubaini vyanzo vya mapato amesema uwepo mradi huo utakuwa chanzo cha ajira kwa watanzania na kuongeza pato la Tanzania pia.
Balozi wa kongo katika ubalozi mdogo wa kongo Kigoma Ricky Mungila Mungie amesema umoja huo utasaidia wasafirishaji kutoka pande zote mbili kufahamu sheria za nchi mbili na itarahisisha usafirishaji.
Akimwakilisha Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Khalfan Moshi ametoa wito kwa pande zote mbili kuendeleza umoja huo na kuzingatia sheria za mipakani na kuweka mifumo mizuri ya mawasiliano kwa wasafirishaji wa Tanzania na Kongo.