

19 February 2025, 13:08
Madiwani kama wawakilihi wa wananchi katika usimamizi wa miradi ya maendeleo wawashirikishe wananchi kufahamu maendeleo ya miradi hiyo
Na Orida Sayon
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru Mkoa wa Kigoma imewataka madiwani katika halmashauri ya wilaya Kigoma Mkoani humo kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo na kuwashirikisha wananchi ili waweze kufahamu miradi iliyopo kwenye maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa dawati la elimu kwa Umma TAKUUKURU Mkoa wa Kigoma Ibrahim Sadiki wakati akzungumza katika baraza la madiwani la halmashuri hiyo lililoketi hii leo kujadili taarifa mbaliimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya Kigoma.
Amesema kuwa ushiriki wa madiwani ni pamoja na kuweka wazi kwa wananchi miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao ili kusaidia kuondoa changamoto za wananchi kulalamiikia ukosefu wa huduma bora kwenye maeneo yao.
Sauti ya Mkuu wa elimu kwa umma TAKUKURU.
Aidha amesema kama taasisi wamekuwa wakiendelea kufuatilia mnyororo wa thamani ya miradi na viwango vinavyotakiwa ili kuhakikisha kunakuwa na miradi yenye tija na manufaa kwa wananchi.
Sauti ya Mkuu wa dawati la Elimu kwa umma TAKUKURU
Naye Katibu Tawala halmashauri ya wilaya Kigoma Mganwa Nzota amesema ni wajibu kwa madiwani na watumishi wa umma kushirikiana na wananchi katika kusimamia utekelezaji wa miradi inakuwa ikiendeshwa kwenye maeneo ya utala wao.