

4 February 2025, 09:24
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Tanzania kanda ya kigoma Agostine Rwezile ameomba kufanyika kwa marekebisho ya sheria ya hukumu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao.
Na Orida Sayon
Amebainisha hayo mapema leo katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya sheria yaliyofanyika katika mahakama kuu kanda ya kigoma nakuzindua rasmi shughuli za kimahakama ambapo amesisitiza kufanya utekelezaji wa hukumu kwa wakati huku kutekeleza hukumu dhidi ya serikali ikiwa miongoni mwa changamoto.
Aidha ametoa rai kwa watumishi wa mahakama na taasisi zinazosimamia haki madai kuzingatia weledi ,uadilifu na uwajibikaji wa majukumu yao huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watumishi wa maswala ya utatuzi wa migogoro kusaidia upatikanaji wa haki kwa wakati
Akitoa risala kwa mgeni rasmi wakili wa serikali mwandamizi Geoge Kalenda kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa serikali amesema katika kuendea safari ya Tanzania ya 2050 taasisi zinazosimamia haki madai zinapaswa kuwa nyenzo ya kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuzingatia haki, na utwala bora na kisheria.
Baadhi ya wananchi walihudhuria katika maadimisho hayo akiwemo msaidizi wa kisheria kutoka Paralega organization wakawa na kusema juu ya utendaji wa shuguli za kimahakama na ushirikiano wao kwa mahakama.