Joy FM

Waziri wa uvuvi na mifugo aeleza serikali kuwawezesha wavuvi Kigoma

21 January 2025, 14:23

Waziri wa  Mifugo  na Uvuvi Dkt. Ashatu Kijaji, Picha na Mtandao

Serikali imesema itaendelea kuwawezesha wavuvi na wachakataji wa mazao ya uvuvi ili kuwasaidia kupata mazao yenye ushindani na kuongeza thamani.

Na Tryphone Odace – Kigoma

Waziri wa  Mifugo  na Uvuvi Dkt. Ashatu Kijaji amewasili Mkoani Kigoma na kupokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa na kueleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuendelea kuwawezesha wavuvu kufanya shughuli zao.

Awali akitoa Taarifa ya kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Uvuvi mkoani Kigoma, Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema soko la mazao ya Samaki kwa mkoa wa Kigoma limeendelea kukua na kuleta tija kwa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo.

Aidha Rugwa amesema kwa kushirikiana na wataalam wa uvuvi, mkoa unaendelea kuhamasisha wananchi kujikita katika uvuvi wa kutumia vizimba ili kuongeza uzalishaji wa samaki pamoja na kulinda Mazingira katika Ziwa Tanganyika na kulifanya kuwa endelevu.

Kupitia ziara hiyo Mhe. Waziri Dkt. Kijaji atazindua kiwanda cha kuchakata Samaki na dagaa cha Kampuni ya LIFA  sambamba na kutembelea vizimba vya kufugia samaki eneo la Katabe Beach Manispaa ya Kigoma Ujiji.