Joy FM

Akina mama watakiwa kuheshimu wenza wao

14 January 2025, 14:09

Waumi wa kanisa la P.A.G Katubuka wakimkabidhi Mchungaji wa kanisa gari, Picha na Lucas Hoha

Ni katika Sherehe Maalumu ya kumkabidhi zawadi ya Gari Askofu mstaafu wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God Tanzania P.A.G Michael Kulwa ambayo imenunuliwa na idara ya akina Mama wa Kanisa

Na Lucas Hoha

Idara ya akina Mama  wa Kanisa la Pentecostal Assemblies Of God Tanzania P.A.G Katubuka  Manispaa ya Kigoma Ujiji, wametakiwa kuwa na mshikamano na kuwaheshimu wenza wao ili Mungu aweze kubariki kazi  za mikono yao.

Mkurugenzi wa Idara ya Umoja wa akina Mama Taifa WWK  Bi. Ester  Bunga ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha akina Mama kutimiza wajibu wao katika familia kwani wapo baadhi ya wanawake baada ya kupata mafanikio wanafanya mambo yasiyofaa.

Sauti ya Mkurugenzi idara ya wamama Taifa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Umoja wa akina Mama Kanisa la P.A.G Katubuka Ombeni Simion Kulana amesema wamekumbana na changamoto mbalimbali wakati wakitekeleza wazo la kununua gari, huku akimshukuru Mungu ambaye amewawezesha kufanikisha wazo hilo.

Sauti ya Mkurugenzi idara ya kinamama kanisani

Akizungumza kwa niaba ya wakina Mama wa Kanisa hilo katibu wa kanisa hilo Ester Isaya amesema ununuzi wa gari hilo umegharimu jumla ya milioni 16 na kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kanisa hilo ili wapate Baraka

Sauti ya katibu wa kanisa

Awali akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa gari hilo Askofu mstaafu wa Kanisa la P.A.G Mchungaji Michael Kulwa pamoja na mambo mengine ameshukuru Idara ya akina Mama kwa heshima hiyo ambayo wamemfanyia na kuwa ataendelea kumtumikia Mungu  kwa utiii na kuwaheshimu watu wengine.

Sauti ya Askofu mstaafu Michael Kulwa