DC Kigoma ashughulikia changamoto za bodaboda
11 January 2025, 12:19
Siku chache baada ya madereva pikipiki maarufu bodaboda mjiji Kigoma kufanya maandamano kufuatia Oparesheni ya Jeshi la Polisi ya kamatakamata madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani iliyosababisha vurugu hatimaye Mkuu wa wilaya Kigoma ameitisha kikao na madereva hao ambapo amesikiliza changamoto zao.
Na Josephine Kiravu – Kigoma
Miongoni mwa ahadi alizotoa ni pamoja na kuwapeleka chuo cha veta madereva ambao hawana leseni ili waweze kusoma na kupata vyeti vitakavyowawezesha kupata leseni.
Kufuatia maandamano ya madereva pikipiki maarufu kama bodaboda hapo Jana, Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua amezungumza na madereva hao na kuwaahidi kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo ukamataji wa kutumia nguvu pamoja na kuwatafutia nafasi kwenye chuo cha ufundi Kwa gharama ya shilingi elf 30 ili kila dereva apate Cheti kitakachomsaidia kupata leseni.
Nao baadhi ya madereva wa pikipiki wameishukuru Serikali huku wakimtaka mkuu wa wilaya kuona haja ya kuzungumza na jeshi la polisi wasiendelee kuwakamata kipindi hiki wanapotafauta vyeti ili wapate leseni za udereva.