Joy FM

Wadau watakiwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji

6 January 2025, 12:15

Pichani ni mwalimu wa shule ya msingi Kisuma Yusuph Ibrahimu akiwa na walimu wa shule ya msingi Rungwe mpya Agatha Chendro na mkuu wa shule ya msingi Kabanga Happiness Ludovic Boy kulia ni mzazi wa mwanafunzi mwenye ulemaavu baada ya kukabidhiwa kitimwendo(wheelchair),-Picha na Hagayi Ruyagila.

Katika kuhakikisha mtoto mlemavu kupata elimu na kutimiza ndoto zao wadau wa maendeleo na wazazi kuibua na kuwatoa nje watoto hao ili kupata haki ya elimu.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wadau wa maendeleo wilayani Kasulu mkoani Kigoni wametakiwa kuwasaidia vitimwendo (wheelchair) watoto wenye ulemavu ili waweze kuendelea na masomo kwa lengo la kutimiza ndoto zao.

Hayo yamejiri baada ya kampuni ya Elvee mediwears kutoa msaada wa viti mwendo viwili kwa mwalimu wa shule ya msingi Kisuma halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Mwl, Yusuph Ibrahimu ili aweze kuwakabidhi wanafunzi wawili wenye mahitaji maalumu kutoka kijiji cha Zeze na Kijiji cha Rugwe mpya.

Mwl, Yusuph akikabidhi vitimwendo hivyo kwa watoto hao amesema lengo la kuwasaidia ni kuwapa urahisi wa kupata mahitaji yao ya kila siku.

Sauti ya Mwalimu Yusuph Ibrahimu

Kwa upande wake Mwalimu wa kitengo maalum katika shule ya msingi Rungwe mpya Agatha Chendro na Mwalimu mkuu shule ya msingi Kabanga Mazoezi Happines Ludovic Boy licha ya kutoa shukurani zao kwa wahisani hao wamewasihi wazazi na walezi kutowafungia ndani watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata elimu itakayowasaidia kutimiza ndoto zao.

Sauti za walimu

Pichani ni Mwalimu Yusuph Ibrahim akiwa na mwanafunzi aliyekabidhiwa kitimwendo,-Picha na Hagai Ruyagila.

Baadhi ya wazazi wa watoto hao akiwemo Juma Ndize kutoka kijiji cha Zeze na Aneth Ruhonyi kutoka kijiji cha Rungwe mpya wameeleza namna walivyopokea msaada huo wakati huo mmoja wa watoto waliopatiwa msaada huo Ndize Juma kutoka Kijiji cha Zeze akaelezea furaha yake baada ya kukabidhiwa kitimwendo chake.

Sauti za Wazazi na Mtoto  

Watoto waliokabidhiwa viti mwendo ni wawili ambao ni Ndize Juma kutoka Kijiji cha Zeze anayejiadaa kujiunga na kidato cha kwanza na Samweli Petro kutoka kijiji cha Rugwe Mpya anayejiandaa kuanza masomo awali.