Joy FM

Zaidi ya matukio ya ukatili 1900 yameripotiwa Kigoma

11 December 2024, 13:23

Afisa ustawi wa jamii Mkoani Kigoma Bw. Petro Bwanji, Picha na Emmanuel Kamangu

Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kushirkiana kutoa elimu na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili ambavyo vinaonekana kuendelea kuongezka Mkoani Kigoma

Na Emmanuel Kamangu – Kasulu

Zaidi ya matukio 1900 ya ukatili kwa wanawake na watoto kwa mwaka 2022/2023  Mkoani Kigoma yameripotiwa  ongezeko hilo likichangiwa na mumomonyoko wa maadili unakua kwa kasi katika jamii.

Amebainisha hayo afisa ustawi wa jamii Mkoani Kigoma Bw. Petro Bwanji Katika kilele cha Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na kubainisha kuwa matukio ya ukatili  wa utelekezaji yameongezeka kwa kasi ikichangiwa na maadili kuporomoka katika jamii.

Sauti ya afisa ustawi wa jamii Mkoani Kigoma Bw. Petro Bwanji

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika maadhimisho haya Daktari  Baraka Endrew kutoka hospital ya rufaa ya Mkoa wa kigoma maweni amesema kuna ongezeko kubwa la matukio ya ukatili hivyo kuna kila sababu za wazazi kuhakikisha wanasimamia vyema swala la malezi.

Sauti ya Daktari  Baraka Endrew kutoka hospital ya rufaa ya Mkoa wa kigoma maweni

Aidha Mtalamu wa masuala ya kijinsia kutoka taasisi ya Jane Goodall Bw. Nyanzandoba John amesema jamii kwa ujumla inawajibu wa kutoa taarifa  za vitendo vya ukatili kwa vyombo vinavyohusika na kumlinda mwanamke na mtoto ili kuendelea kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili.

Sauti ya Mtalamu wa masuala ya kijinsia kutoka taasisi ya Jane Goodall Bw. Nyanzandoba John
Mtalamu wa masuala ya kijinsia kutoka taasisi ya Jane Goodall Bw. Nyanzandoba John

Baadhi ya wananchi sambamba na viongozi kutoka asasi mbali mbali wilayani kasulu ambao wameshiriki maadhimisho haya wamesema elimu ambayo wamepata itawasaidia kuendelea kusimama kidete kumlinda mwanamke na mtoto.

Sauti ya Mtalamu wa masuala ya kijinsia kutoka taasisi ya Jane Goodall Bw. Nyanzandoba John

Maadhimisho  haya huanza Novemba  25na kilele chake hufanyika disemba 10 kila mwaka ambapo  kimkoa yamefanyika katika mji wa kasulu  yakibwebwa na kaulimbiu  isemayo kuelekea miaka 30 ya Beijing, chagua kutokomeza ukatili.