Joy FM

Viongozi wa kata, mitaa watakiwa kusimamia usafi wa mazingira

9 December 2024, 15:12

Baadhi ya watumishi wa halmashauri na kamati ya ulinzi na usalama na wananchi wakifanya usafi, Picha na Hagai Ruyagila

Wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia suala la usafi wa mazingira ili kuhakikisha hakuna mlipuko wa magonjwa.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Watendaji wa kata na mitaa halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuhakikisha mitaa yao ina imarishwa katika usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika viongozi wa serikali halmashauri ya mji Kasulu wameshiriki zoezi la usafi wa mazingira ili kuhakikisha maeneo ya kutoa huduma za afya yanakuwa katika mazingira mazuri.

Akizungumza mara baada ya zoezi hio kutamatika mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye amesema viongozi wa mitaa na kata wanalojukumu la kuhakikisha wanaimarisha usafi wa mazingira katika maeneo yao.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye akifyeka majani wakati wa zoezi la usafi, Picha na Hagai Ruyagila

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Kasulu SSP Sango Sango amesema suala usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja hivyo kwa upande wa jeshi hilo wameona ni vyema kujumuika pamoja katika suala la usafi wakati wa sherehe za miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika.

Sauti ya Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Kasulu SSP Sango Sango
SSP Sango Sango Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Kasulu SSP SANGO, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake, katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi, Theresia Mtewele amewataka wananchi kuwa wazalendo katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatunzwa na kutunza mazingira ili kuleta matokeo chanya katika jamii.

Sauti ya Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi, Theresia Mtewele

Usafi huu wa mazingira umejumuisha kamati ya ulinzi na usalama, Wafanyakazi wa halmashauri ya Mji Kasulu pamoja na Wananchi kutoka halmashauri ya Mji Kasulu.