Joy FM

Mme auwa mke wake na mwili kutupwa chooni

4 December 2024, 13:19

Picha ni mwili wa mwanamke aliyefariki baada ya kupigwa na mme wake kisha mwili kutupwa chooni, Picha na Mollovan Chepa

Wakati tukiwa ndani ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na elimu ikiendelea kutolewa bado hali si shwari kwani vitendo hivyo vimeendelea kutokea hasa kwa wanandoa.

Na Mullovan Cheppa – Kigoma

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Dorcas Nyerere mwenye umri wa miaka 20 ameuawa na mwili kutupwa chooni baada ya kupigwa na mme wake Bw. Uwesu Isack chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi katika kitongoji cha mkayogolo kata ya Bitale halmashauri ya wilaya Kigoma.

Ni muonekano wa shimo la choo ulipotupwa mwili wa Dorcas Nyerere anayedaiwa kuuwawa na mme wake, Picha na Mullovan Cheppa

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika kitongoji hicho wameeleza kusikitishwa na tukio hilo.

Sauti ya Baadhi ya wananchi wanaoishi katika kitongoji hicho yalipotokea mauwaji hayo.

Naye Mrakibu Msaidizi wa jeshi la Zima moto na uokoaji Mkoa wa Kigoma Michael Maganga amesema walipokea taarifa ya mwili wa mtu kuonekana kwenye shimo la choo na walifika kwa wakati na kuutoa mwili huo.

Maafisa wa jeshi la zimamoto Mkoa wa Kigoma wakiwa wanaangalia mwili uliotupwa kwenye shimo la choo, Picha na Mullovan Cheppa

Insert……..02 Mkaguzi Zimamoto

Sauti ya Mrakibu Msaidizi wa jeshi la Zima moto na uokoaji Mkoa wa Kigoma Michael Maganga

Hata hivyo jitihada za kumpata kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma ili kuzungumzia tukio hazijazaa matunda licha ya uwepo wa taarifa kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka bw. Uwesu Isack Maarufu Sheikhe Modo  Mwenye Umri wa miaka 30 Mkazi wa Kijiji cha Bitale Wilayani Kigoma kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Doricas Nyerere .