Joy FM

CRDB yakabidhi madawati 40 shule ya msingi kabulanzwili Kasulu

4 December 2024, 12:42

Ni madawati ya yaliyotolewa na Benki ya CRDB ili kuunga mkono serikali kuboresha elimu, Picha na Michael Mpunije

Wadau wa maendeleo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuisadia Serikali kujitokeza kuchangia michango kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa wananfunzi.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Benki ya CRDB kanda ya magharibi imekabidhi jumla ya madawati 40 yenye thamani ya shilingi milioni 4 katika shule ya msingi kabulanzwili kata ya kurugongo halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ili kusaidia wanafunzi  kusoma katika mazingira mazuri.

Kaimu meneja wa Benki ya CRDB kanda ya magharibi Evod Kereti amesema benki hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo na kutatua baadhi ya changamoto katika sekta ya elimu.

Sauti ya Kaimu meneja wa Benki ya CRDB kanda ya magharibi Evod Kereti

Kwa upande wake afisa elimu awali na msingi  halmshauri ya wilaya ya kasulu Bi,Elistina Chanafi amesema shule  ya msingi kabulanzwili ina  zaidi ya wanafunzi elfu 1 hali ambayo imepelekea kuwa  na changamoto mbalimbali ikiwemo madawati ,matundu ya vyoo na nyumba za waalimu huku msaada huo ukitajwa kupunguza uhaba wa madawati  kwa asilimia 47.

Sauti ya afisa elimu awali na msingi  halmshauri ya wilaya ya kasulu Bi. Elistina Chanafi
Wanafunzi wa shule ya msingi Kabulanzwili wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kutoka Benki ya CRDB, Picha Michael Mpunije

Kaimu Mkurugenzi halmshauri ya wilaya ya Kasulu Bw,Ndelekwa Vanica amesema wadau wamaendeleo  wanapaswa kujitokeza kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika halmshauri hiyo kupitia sekta mbalimbali.

Sauti yaKaimu Mkurugenzi halmshauri ya wilaya ya Kasulu Bw. Ndelekwa Vanica

Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac mwakisu ameishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo wa madawati na kumtaka mkuu wa shule hiyo kuhakikisha anasimamia miundombinu ya shule kwa ajili ya manufaa ya wanafunzi na kuhakikisha miundombinu hiyo inadumu kwa muda mrefu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac mwakisu
Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isac Mwakisu kwenye picha na Kaimu Meneja wa CRDB pamoja wanafunzi wa shule ya msingi Kabulanzwili, Picha na Michael Mpunije