Anusurika kifo baada ya kuchomewa ndani na mme wake
29 November 2024, 17:23
Wakati tukiwa kwenye siku 16 za kupinga ukatilii wa kijinsia na elimu kuendelea kutolewa kwa jamii bado ukatilii wa aina mbalimbali umeendelea kufanyika.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Mkapa kata ya Kumnyika halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma amenusurika kifo baada ya kuchomewa ndani ya nyumba na aliyedai kuwa ni mume wake chanzo kikitajwa kuwa ni migogoro ya kifamilia.
Bi. Teudola Mussa mama aliyefanyiwa tukio hilo akizungumza na radio Joy fm amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia novemba 29 na chanzo akidai kuwa ni migogoro ya kifamilia huku akibainisha kuwa vitu vyote vilivyokuwa sebuleni vimeungua kwa moto.
Bi, Vumilia Sanda na Suleiman Rashid ni mashuhuda wa tukio hili.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo SGT Africanus Mrema mkuu wa zimamoto Kasulu amekili kutokea kwa tukio hilo na amewaomba wakazi wa wilaya ya Kasulu pindi wanapokutana na matukio ya namna hiyo watoe taarifa serikaini.