Mkandarasi akabidhiwa mkataba na ramani ya soko la mwanga Kigoma
21 November 2024, 12:54
Mkandarasi anayetajaiwa kujenga soko la mwanga na mwalo wa Katonga Manispaa ya Kigoma Ujiji ametakiwa kuanza ujenzi wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Na Lucas Hoha – Kigoma
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba amekabidhi mkataba, ramani na kuonyesha mipaka ya Soko la Mwanga na Mwalo wa Katonga kwa Kampuni ya ASABHI CONSTRACTORS LIMITED inayoshirikiana na PIONEER BUILDERS LIMITED kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Soko la Mwanga na Mwalo wa Katonga miradi inayotarajia kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 16.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba amesema wamemuelekeza mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia ubora kulingana na mkataba.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mbali na kutoa shukrani kwa serikali kwa ajili ya juhudi za ujenzi wa Soko na Mwalo wa katonga wamesema pindi ujenzi huo utakapokamilika itasaidia uwepo wa mzunguko wa biashara na kuwavutia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.