Wanaccm walia na migogoro ya ardhi na umeme Kigoma
21 November 2024, 10:04
Wakati kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa zikiwa zimenduliwa rasmi, viongozi wa chama cha mapinduzi wameomba serikali kuaidia kutatua changamoto za ukosefu wa umeme na migogoro ya ardhi.
Na Emmanuel Kamangu – Kasulu
Serikali kupitia chama cha mapinduzi ccm imeombwa kumaliza tatizo la umeme pamoja na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza katika maeneo mengi mkoani kigoma.
Amebainisha hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoani kigoma Bw, Jamal Tamimu katika uzinduzi wa kampeni za serikali za mitaa ambao kimkoa umefanyika katika viwanja vya kiganamo wilayani kasulu na kumuomba Comred Christopher Gachuma ambaye amekuwa mgeni rasimi kwa niaba ya waziri mkuu kasimu majaliwa kuhakikisha anafikisha salamu hizo ili changamoto ya umeme na ardhi ipatiwe ufumbuzi.
Kwa upande wake Bw, Christopher Gachuma ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa amesema tatizo la umeme na migogoro ya ardhi ni moja ya mambo ambayo serikali tayari imeshatenga fedha ili kuhakikisha changamoto zote hizo ambazo zimekuwa zikileta shida kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa kigoma zinapatiwa suruhu.
Aidha Bw, Gachuma amesema wananchi mkoani kigoma wanapaswa kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi ccm ili kiendelea kuimalisha hali ya amani na utulivu pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo.
Hata hiyo Bw. Gachuma amesema kutokana na maendeleo ya kutosha ambayo ccm imepeleka kwa wananchi wa mkoa wa kigoma anauhakika wananchi watachagua kwa kishindo viongozi wa vitongoji, mitaa na vijiji wanaotokana na chama cha mapinduzi.