TAKUKURU yawataka wagombea kuepuka rushwa Kasulu
13 November 2024, 13:46
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU katika wilaya ya Kasulu imesema wagombea kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa.
Na Emmanuel Kamangu – Kasulu
Kutokana na umhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi wilayani Kasulu wametakiwa kutokuwachagua wagombea ambao watajihusisha na utoaji rushwa wakati wa kampeni.
Amebainisha hayo kaimu kamanda wa takukulu wilayani kasulu Elimilik Kihundwa wakati akizungumza na redio joy ofisini kwake na kuwasihi wananchi kuachana na zawadi za wagombea zenye viashiria ya rushwa ili kuepuka kuweza kupata viongozi wasiofaa.
Aidha Kamanda kihundwa amewataka wagombea kuacha tabia ya kutoa rushwa wakati wa kampeni kwani kufanya hivo kunaweza kuwanyima fursa ya kuwa viongozi hata kama wamechaguliwa.
Kwa upande wao wananchi wilayani kasulu wamesema wagombea watakaotumia siraha ya kutoa rushwa kama kigezo cha kuchaguliwa watakosa sifa ya kupata kura zao.
Hata hiyo wananchi hao wameongeza kuwa rushwa ni adui wa haki hivyo hawako tayari kupoteza utu wao kwa kupewa chumvi na kanga .