Joy FM

Buhigwe watakaovuruga uchaguzi kukiona cha moto

3 November 2024, 20:39

Mkuu wa wilaya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina na picha, Michael Mpunije

Halmashauri ya wilaya Buhigwe kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Kanali Michael Ngayalina imesema imejianda vyema kuhakikisha ulinzi unaimarika katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa.

Na Michael Mpunije – Buhigwe

Kamati ya Usalama ya wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imesema imejipanga kuimarisha ulinzi na usalama wilayani humo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili zoezi hilo lifanyike kwa Amani.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina wakati akizungumza na Kipindi hiki Ofisini kwake na kueleza namna walivyojipanga kuhakikisha zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa linafanyika kwa amani kwa kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa za kuchagua anashiriki kikamilifu katika zoezi hilo akiwa na amani ya Kutosha.

Kanali Ngayalina

Aidha Kanali Ngayalina amesema Jeshi la Polisi wilayani humo limeendelea na kufanya mazoezi ya Utayari kwa lengo la kuimarisha usalama katika maeneo ya kupiga kura huku akiwatoa hofu wananchi kuwa zoezi hilo litafanyika kwa kadri maelekezo ya Serikali yatakavyotolewa nakuwaataka wananchi kushiriki katika uchaguzi huo kwa lengo la kuwachagua viongozi mbalimbali wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo.

Kanali Ngayalina

Sanjari na hayo amewasisitiza wagombea na wafuasi wa vyama vya Siasa kufanya kampeni za Staha wakati utakapowadia ili kuepuka kujihusisha katika Uvunjifu wa Amani Ili kila mmoja Kutimiza wajibu wake kwa Kufuata Sheria za Nchi.

Kanali Ngayalina