Joy FM

Nyumba 10 zimebomoka kutokana na mvua Kasulu

1 November 2024, 12:15

Muonekano wa nyumba zilizoezuliwa na mvua wilayani kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Kigoma zimesababisha baadhi ya nyumba kubomoka na mali za watu kuharibiwa.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Zaidi ya nyumba 10 katika mtaa wa mkombozi kata ya murusi halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma zimebomoka na nyingine kuezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha oktoba 29 mwaka huu.

Paa la nyumba likuwa chini baada ya kupeperushwa na upepo ulioambatana na mvua, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa mkombozi wakieleza namna walivyoshuhudia upepo mkali na kuasababisha madhara hayo ambayo yamesababisha baadhi ya wananchi hao kukosa makazi yakuishi. Timotheo Maliatabu, Selina Kahendabia , Josephati Leonard na Zelda James ni baadhi ya wahanga wa mvua hiyo.

Sauti ya Baadhi ya wananchi wa mtaa wa mkombozi Wilayani Kasulu
Ni muonekano wa paa la nyumba lililoezuliwa kufuatia mvua zilizonyesha huko wilayani Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Afisa mtendaji wa kata ya Murusi Omary Sebabili amezulu katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ili kuona uwezokano wa kutoa msaada wa awali kwa wahanga waliokubwa na kadhia hiyo.

Sauti ya Afisa mtendaji wa kata ya Murusi Omary Sebabili

Mbali na nyumba hizo kubomoka pia baadhi ya nyumba zilizojaa maji ambapo afisa afya, mazingira na mkuu wa kitengo cha udhibiti wa taka halmashauri ya Mji Kasulu Msafiri Charles ameeleza madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza.

Sauti ya afisa afya, mazingira na mkuu wa kitengo cha udhibiti wa taka halmashauri ya Mji Kasulu Msafiri Charles
Muonekano wa iliyobomolewa na mvua wilayani Kasulu, Picha na Hagai Ruygagila