Wazee walia na unyanyasaji kwenye jamii Kigoma
24 October 2024, 11:37
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wamesema wataendelea kuweka mazingira bora na rafiki kwa wazee mkoani Kigoma ili wajione kuwa sehemu ya jamii.
Na Winfrida Ngassa – Kigoma
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Mohamed Chuachua amekemea vikali vitendo vya ukatili dhidi ya wazee na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wananwake na watoto.
Hayo yanajiri katika Sherehe ya maadhimisho ya siku ya wazee Duniani katika kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha SILAB kilichopo Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo amesema serikali haitakuwa tayari kufumbia macho vitendo hivyo kwani vitendo hivyo ni udhalilishaji wa kiutu kama anavyoeleza.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi afisa ustawi mfawidhi makao SILAB bwana Frednand Charles amesema makao hayo ya wazee ya na jumla ya wazee 26 kwa sasa kati yao wanaume ni 15 na wanawake ni 11 kati ya idadi hiyo kuna walemavu wa macho, viungo na wenye ukoma.
Afisa huyo mfawidhi ameendelea kumweleza Mkuu wa Wilaya hiyo kuwa, katika makao hayo ya SILABU mbali na mafanikio waliyo nayo bado makao hayo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama anavyoeleza.
Naye mwakilishi wa wazee Ester Lukonya mbele ya mgeni rasmi ameishukuru serikali na shirika la Joy in the HARVEST kwa kuendelea kuwahudumia wazee hao kwani wazee hao wanahitaji msaada wa kutosha ili Kuendelea kufurahia maisha yao, Huku Mkurugenzi wa Radio Joy na Joy In the Harvest Bwana Mwenge Muyombi amesema kama shirika litaendelea kuwashika mkono ili kuweza kutimiza lengo na adhma ya wazee hao.
Makao hayo ya wazee wa Silabu yamedumu tangu mwaka 1971 na kabla ya hapo makao haya yalikuwa yanatumika kama kituo cha kuwakusanya na kuwasafirisha watu ambao walikuwa wanaenda kufanya kazi kwenye mashamba ya mikonge maarufu kama manamba katika mikoa ya Tanga na Morogoro.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni Tuimarishe huduma kwa wazee, wazeeke kwa heshima.