Joy FM

Askofu Emmanuel Bwatta ajiandikisha kwenye daftari la mkaazi Kasulu

18 October 2024, 17:30

Askofu wa Kanisa la anglikana dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwata amewataka wananchi kujiandikisha ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mita.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wito umetolewa kwa wananchi wa wilaya ya Kasulu Mkoni Kigoma kutumia muda uliobaki kujitokeza kujiandikisha katika daftari la Mpiga kura ili kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27, 2024.

Mhashamu askofu Emmanuel Bwatta wa Kanisa la anglikana dayosisi ya western Tanganyika ametoa wito huo, mara baada ya kukamirisha zoezi la kujiandikisha katika kituo cha kata ya Murubona kilichopo katika shule ya msingi Murubona.

Mhashamu askofu Emmanuel Bwatta wa Kanisa la anglikana dayosisi ya western Tanganyika, Picha na Hagai Ruyagila

Baada ya kukamilisha zoezi hilo amewasihi wananchi kujiandikisha ili kupata fursa ya kuchagua viongozi wa ngazi ya mtaa kwani muda uliobaki kwa ajili ya kujiandikisha ni mchache.

Sauti ya Mhashamu askofu Emmanuel Bwatta wa Kanisa la anglikana dayosisi ya western Tanganyika

Aidha askofu Bwatta amewahimiza vijana kuonyesha uzalendo kwa kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili kuchagua viongozi watakao waletea maendeo kuliko kulalamikana na wakati hawajajiandikisha.

Sauti ya Mhashamu askofu Emmanuel Bwatta wa Kanisa la anglikana dayosisi ya western Tanganyika

Kwa upande wake Bi. Jusirini Bwatta mke wa askofu Emmanuel Bwatta amewaomba akinamama kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha na kuachana kupuuzia suala hilo.

Bi. Jusirini Bwatta mke wa askofu Emmanuel Bwatta akiwa anajiandikisha katikadaftari la mkaazi, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Bi. Jusirini Bwatta mke wa askofu Emmanuel Bwatta

Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha wamezungumzia umuhimu wa kujiandikisha na wengine kujitokeza ili kuchagua viongozi.

Sauti ya baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha

Kulingana na tangazo la wizara ya nchi ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikai za mitaa TAMISEMI, Mwisho wa wananchi kujiandikisha ni oktoba 20, 2024 na zoezi la kupiga kura litafanyika novemba 27, 2024.