Joy FM

RC Kigoma ahamasisha wananchi kutumia muda uliobaki kujiandikisha

17 October 2024, 13:19

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali msitaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye kujiandikisha daftari la mkaazi, Picha na Ofisi ya mkuu wa mkoa

Ukosefu wa Elimu Kwa Wananchi Mkoani Kigoma, Umepelekea kuchanganya zoezi la kuandikisha wapiga kura, na vitambulisho vya mpiga kura, na huenda wengi wao wakakosa sifa za kuwa na uhalali wa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa kushidwa kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amejiandikisha katika daftari la mkaazi la mpiga kura katika mtaa wa shede kata ya Kigoma Mjinina kutoa wito kwa wakazi mkoani kigoma kutumia muda uliobakikujitokeza na kujiandikisha ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi wa serikli za mitaa novemba 27, 2024.

Na Kadislaus Ezekiel – Kigoma

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina Jenerali msitaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mheshimiwa Thobias Andengenye, amesema hayo, mara baada ya kumaliza kujiandikisha katika kituo cha kata ya Kigoma, na kueleza wananchi kutojiandikisha wakichanganya na vitambulisho vya mpiga kura.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina Jenerali msitaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, Picha na Ofisi ya mkuu wa mkoa

“Jiandikisheni kwa maana kwa zoezi hili vile vitambulisho havitatumika katika uchaguzi wa huu wa serikali za mitaa kila mmoja akijitokeza tutakuwa na nguvu ya kuweza kuwachagua viongozi tunaowataka”

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali msitaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye

Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha, wameeleza umuhimu wake, na kuwataka wananchi wengine kujitokeza ili kuwa na uhalali wa kuchaguza viongozi.

Sauti ya baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha