Wananchi Kibondo wajitokeze kujiandikisha daftari la kura
16 October 2024, 14:35
Zikiwa zimesalia siku nne pekee kabla ya zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mkaazi kwa ajili kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa viongozi wa dini wameendelea kuhamasisha wananchi kutumia muda uliobaki kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.
Na James Jovin – Kibondo
Viongozi wa dini wilayani Kibondo mkoani Kigoma wamewataka wananchi kuendelea kujiandikisha kwa wingi katika siku hizi chache zilizobaki ili kuweza kuchagua viongozi wa serikali za mitaa wenye sifa za kuongoza na kuleta maendeleo katika jamii.
Viongozi hao wa dini wamesema hayo wakati wa zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa linaloendelea kote nchini na kwamba wananchi wanapaswa kulichukkulia kwa umuhimu wake
Aidha asikofu wa kanisa anglikana Dayosisi ya Kibondo Sosipater Ndenza pamoja na askofu wa kanisa la EAGT Kanda ya magharibi Dr. Wandali Ndonka wamesema kuwa ili kupata viongozi bora katika serikali za mitaa ni wajibu wa kila mwananchi kujiandikisha na kupiga kura
Sauti ya viongozi wa dini Sospeter Ndenza na Wandali Ndonka
Kwa upande wake katibu wa bakwata wilaya ya Kibondo shehe Maneno Yahya Rugage amewakumbusha waumini wa dini zote kuhakikisha wanajiandikisha na kuchagua kwa kuwa uchaguzi huu ni tofauti na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
Suti ya shekhe Maneno Yahya
Nae mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amesema licha ya kwamba wananchi wengi kwa sasa wako katika maandalizi ya msimu wa kilimo lakini wanapaswa kujiandikisha kwa kuwa ni muda mfupi kujiandikisha na kisha wanaweza kuendelea na shughuli zao
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kibonndo kanali Agrey Magwaza
Katika wilaya ya Kibondo jumla ya vituo 422 vitahusika kuandikisha wapiga kura serikali za mitaa katika kata zote 50 zilizoko ndani ya wilaya hiyo ambapo Zaidi ya watu laki moja wnatarajiwa kuandikishwa.W