DC Kasulu: Jiandikisheni ili muwe na sifa za kupiga kura
14 October 2024, 12:29
Wananchi wamehimizwa kuendelea kujitkeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la makazi ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.
Na Lucas Hoha – Kasulu
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu amewaomba wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza kikamilifu kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili wawe na sifa ya kupiga kura kwa kuwachagua viongozi wao wa serikali mitaa ifikapo Novemba 27 mwaka huu 2024.
Mwakisu ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la uandikishaji wa daftari la mkazi kwa wananchi wa mji wa kasulu, amesema zoezi hilo linalowahusisha wananchi wenye umri wa kuanzia miaka 18 nakuwa atakayeshindwa kujiandikisha kwenye daftari hilo atakosa sifa za kupiga au kupigiwa kura kwenye uchaguzi huo.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu Vumilia Julius amesema maandalizi ya vituo kwa ajili ya kazi hiyo yamekamili, nakuwa jumla ya vituo 225 vitatumika kujiandikisha kwenye daftari la mkazi.
Nao baadhi ya wananchi wa Mji wa Kasulu ambao wamejitokeza kujiandikisha, wamesema wamejiandikisha kwenye daftari hilo kwa ajili ya kupiga kura, kwani wanatambua mchango wa viongozi wa serikali za mitaa katika harakati za kuleta maendeleo.
Kwa mjibu wa Msimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu wanatarajia kuandikisha watu laki 120,700