Joy FM

Prof. Ndalichako awataka vijana kugombea nafasi za uongozi

14 October 2024, 11:53

Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa eneo la Shayo kata ya Mrusi. Picha na Emmanuel Kamangu

Wakati zoezi la kujiandkisha kwenye daftari la makazi kwa ajili ya wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa vijana wameaswa kujitokeza na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Na Emmanuel Kamangu – Kasulu

Vijana na wanawake kata yaMrusi halmashauri ya mji wa Kasulu wametakiwa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uatakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini Prof. Joyce Ndalichako wakati akizungumza na wananchi wa eneo la Shayo kata ya Mrusi halmashauri ya mji wa Kasulu ambapo amewasihi vijana na wanawake kugombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini Prof. Joyce Ndalichako

Aidha Prof. Ndalichako amesema katika kata ya Mrusi mwenendo wa wananchi kujisajili katika daftari la mpiga kura hauridhishi na kuwaomba wananchi na watumishi mbalimbali wa serikali kujisajili ili kupata haki ya kuwachagua viongozi bora.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini Prof. Joyce Ndalichako

Kwa upande  wake mjumbe wa Mkutano Mkuu Cham Cha Mapinduzi CCM wilaya Bw. Lucas Gervas ambaye  ameambatana na mbunge amesema njia sahihi ya kupata viongozi bora ni kujiandikisha ili kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa maendeleo ya Taifa.

Sauti ya mjumbe wa kutano mkuu CCM wilaya Bw. Lucas Gervas

Hata hivyo wananchi ambao wamejitokeza katika mkutano huu wa hadhara wamemuahidi pro, ndalichako kujitokeza kikamilifu kujiandikisha ili wasikose haki ya kuchagua viongozi bora.

Wananchi wa kata ya Mrusi wakiwa katika maandamano ya kupokea Prof. Ndalichako. Picha na Emmanuel Kamangu