Miradi ya bilioni 4 yakaguliwa na kuzinduliwa Kibondo
23 September 2024, 15:58
Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 umekimbizwa wilayani Kibondo mkoani Kigoma na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Na James Jovin – Kibondo
Jumla ya miradi sita yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4 imekaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
Akisoma taarifa ya miradi hiyo mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amesema kuwa miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na miradi ya maji, afya, barabara na elimu.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la muhambwe Dr. Frolence Samizi amesema kuwa serikali inaendelea kufanya kazi kubwa ya kuboresha miundo mbinu na kukuza uchumi hasa katika sekta ya elimu ambapo karibu kila kata sasa ina shule ya sekondari.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu . Godfrey Eliakimu Mnzava amewataka viongozi katika wilaya ya Kibondo kusimamia vyema fedha zinazoletwa na serikali hasa katika sekta ya elimu ili kuboresha taalumu na elimu kwa ujumala.