Wakristo watakiwa kuliombea taifa amani Kasulu
23 September 2024, 13:26
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Kasulu amewataka wakristo kuendelea kuliombea taifa na mshikamano hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Na Emmanuel Kamangu – Kasulu
Waamini wa kanisa la Anglikana wilayani Kasulu wametakiwa kuendelea kuwaombea wachungaji wastaafu ili waendelee kuwa na ari ya kumtumkia Mungu kwa moyo wao wote.
Ameeleza hayo Mwenyekiti wa Halamashauri ya Mji wa Kasulu Bw. Noel Hanula akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bwami hotel Dubai Chocha katika hafla ya kumuaga mchungaji Amon Ndenza wa Kanisa la Anglikana Parishi ya Mwanga Msanga wilayani Kasulu na kumpongeza mchungaji Ndeza kwa utumishi wake mwema huku akiwaomba viongozi wa dini kuiombea Tanzaia ili iendelee kuwa na amani na utulivu hasa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa hapo Novemba mwaka huu.
Mchungaji Ndeza amehudumu katika utumishi wake kwa takribani miaka 39 akishirikiana kwa ukaribu na mama mchungaji Bi Leonita Mahobe wamesimulia safari ya utumishi wao ambayo ilikuwa ya neema huku wakiwashukuru waamini kwa kuwatia moyo wakati wote mpaka kufika sasa wanapo staafu.
Kwa upande wao wamini wa kanisa la angrikani wamesema mch ndenza katika huduma yake ya utumishi amekuwa mtu wa haki na mwenye upendo huku wakimuombea afya njema.
Aidha Mkurugenzi wa kanda ya heru juu Mch, Pison Elia akiwa katika hafla hiyo amesema mchungaji ndenza kila alipo pita kufanya huduma ameacha alama kubwa kwa kuwaletea waamini maendeleo ya kiroho na kimwili.