Shilingi milioni 950 zakamilisha barabara mjini Kasulu
18 September 2024, 17:06
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024, Godfrey Eliakim Mnzava amemtaka meneja wa TARURA wilaya Ksulu kuhakikisha anaweka taa kwenye barabara ambayo imejenwa kwa gharama ya shilingi milioni 950.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Jumla ya shilingi milioni 950 kutoka serikali kuu kupitia mfuko wa Jimbo la Kasulu Mjini na tozo zimetumika kujenga mradi wa barabara kwa kiwango Cha lami GTZ na Kiganamo Bogwe yenye kilometa 1.1. katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kiwango Cha lami meneja wa Tarura wilaya ya Kasulu Mhandisi Senzia Maenda amesema lengo la ujenzi huo ni kupunguza msongamano wa magari katika baadhi ya barabara mjini kasulu.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Eliakim Mnzava amekagua na kuweka jiwe la msingi katika barabara hiyo ambapo ametoa maelekezo kukamilisha vitu vilivyobakia ili uweze kukamilika kama ilivyo pangwa.
Mwenge wa uhuru wa mwaka 2024 umebebwa na kaulimbiu isemayo tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Kwa ujenzi wa taifa endelevu