Joy FM

RUWASA Kasulu yatakiwa kukamilisha mradi wa maji

18 September 2024, 15:15

Kiongozi wa mwenge wa uhuru itaifa akizungumza mara baada ya kutembelea mradi wa maji  kata ya kimobwa Mjini Kasulu, Picha na Emmanuel Kamangu

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024, Godfrey Mnzava amemtaka Mkurgenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira katika halmashauri ya mji wa kasulu kusimamia ujenzi wa mradi wa maji Kimobwa ili uweze kukamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.

Jumla ya miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya  shilingi Bilioni 2 imepitiwa na mwenge wa uhuru katika halmashauri ya mji wa kasulu ikiwemo ujenzi wa mradi wa maji ambapo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava amemtaka mkurugenzi wa mamalaka ya maji mjini kasulu kuharakisha mradi huo