Walimu watoro kazini kuchukuliwa hatua Kibondo
13 September 2024, 09:31
Baraza la madiwani wilayani Kibondo Mkoani Kigoma limesema litawachukulia hatua za kinidhamu walimu wote ambao wamekuwa hawakai kwenye vituo vyao vya kazi hasa muda wa masomo na kwenda kufanya biashara
Na James Jovin – Kibondo
Serikali wilayani Kibondo mkoani Kigoma imewaonya baadhi ya walimu wanaofanya shughuli za ujasiliamli na bodaboda wakati wa kazi na kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Habili Maseke wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa IOM mjini Kibondo.
Aidha bw. Habili amesema kuwa baadhi ya shule walimu karibu wote wamekuwa wakiondoka kwenye shughuli zao na kuwaachia shule wanafunzi ambao ni viongozi ili muda wa kutawanyika ukifika waweze kutawanya wenzao swala ambalo si sawa kwa mujibu wa maadili ya kazi za umma.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Deocles Rutema amesema kuwa ikama ya walimu haitoshi lakini pia uko mpango wa kuwasimamia walimu hao ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi.