Joy FM

Miradi ya bilioni 6 kuzinduliwa na wenge wa uhuru Kasulu

12 September 2024, 16:00

Mkuu wa wilaya Kasulu Kanasli Isack Mwakisu akizungumza na wanahabari, Picha na Hagai Ruyagila

Mkuu wa wilaya Kasulu Mkoani Kigoma amewataka wananchi kujitokeza kuupokea mwenge wa uhuru utakapowasili wilayano na kushuhudia miradi ya maendeleo ikizinduliwa na kuanza kutoa huduma kwa jamii.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Mwenge wa uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuwasili wilayani Kasulu mkoani Kigoma septemba 18 2024 kuzindua na kutembelea miradi mbalambali ya maendeleo yenye zaidi ya shilingi bilioni 6

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.

Amesema mwenge wa uhuru utapokelewa katika shule ya msingi Tulieni iliyopo kata ya heru juu ukitokea wilayani Buhigwe ndipo utaendelea na uzinduliwa wa miradi ya afya, maji, elimu, mazingira na barabara na kuelekea katika uwanja wa umoja uliopo Halmashauri ya mji Kasulu kwa ajili ya mkesha.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Isack Mwakisu

Aidha Kanali Mwakisu anaendelea kuzungumzia miradi ya maji itakazo zinduliwa wilayani Kasulu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu

Na hapa Kanali Mwakaisu amewaomba wananchi wa wilaya ya Kasulu kuupokea mwenye wa uhuru katika maeneo yote utakapopita kuzindua miradi au kutembelea miradi ndani ya wilaya hiyo.

Mwenge wa uhuru wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   unatarajiwa kukimbizwa ndani ya wilaya ya Kasulu kwa takribani kilometa 99.86