Serikali yafafanua zahanati kutumika bila kusajiliwa Kasulu
6 September 2024, 11:53
Kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Bw.Mberwa chidebwe imeendelea kushikiria msimamo wake wa kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chekenya.
Na Michael Mpunije – Kasulu
Serikali katika Halmashauri ya wilaya ya Kasulu imetolea Ufafanuzi suala za ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chekenya kata ya Kurugongo ambayo ilisajiliwa wakati ujenzi wake ukiwa bado haujakamilika.
Katika taarifa ya awali kwa Waandishi wa habari ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kasulu Mberwa Abdalla chidebwe ilionyesha kamati ya siasa wilayani humo kutoridhishwa na ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha chekenya ambayo imesajiliwa na kwamba imekuwa ikipokea vifaa tiba wakati ujenzi wake ukiwa bado haujakamilika.
Kwa upande wake mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Kasulu Dkt Robert Rwebangira amesema zahanati hiyo haijasajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi bali wamefanya hivyo kwa kufuata utaratibu wa serikali.
Naye mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu ameeleza sababu za kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha chekenya.
Hata hivyo kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Bw.Mberwa chidebwe imeendelea kushikiria msimamo wake wa kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa zahanati hiyo na kutaka kamati kutoa taarifa kamili kuwa ni lini ujenzi huo utakamilika ili wananchi waweze kupata huduma.