CCM yatilia shaka ujenzi wa zahanati pesa ikiliwa
5 September 2024, 16:23
Wananchi wa kijiji cha chekenya wilayani mkoani kigoma huenda wakawa wanapitia shuruba za kukosa huduma za afya baada ya zahanati iliyopo kijijini humo kusajiliwa kuwa inatoa huduma huku ikiwa haijakamilika na seriakli ikiitengea bajeti kuwa miongoni mwa zahanati zinazotoa huduma
Na Michael Mpunije – Kasulu
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi wilayaya Kasulu Mkoani Kigoma imeeleza kutoridhishwa na ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Chekenya kata ya Kurugongo kutokana na zahanati hiyo kusajiliwa wakati ujenzi wake ukiwa bado haujakamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea zahanati hiyo katika ziara ya chama cha mapinduzi ya kutembelea miradi ya maendeleo wilayani humo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, CCM wilaya ya kasulu Mberwa Abdala chidebwe amesema hawajaridhishwa na ujenzi wa zahanati hiyo.
Bw. Chidebwe amesema zahanati hiyo imesajiliwa tangu mwaka jana na kwamba vifaa tiba vimekuwa vikipelekwa katika zahanati hiyo licha ya ujenzi kutokamilika jambo ambalo hupelekea wananchi kushindwa kupata huduma kwa wakati.
Ujenzi wa zahanati ya kijiji cha chekenya kata ya Kurugongo ulianza kutekelezwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2021 kuanzia hatua ya msingi hadi ukuta ambapo serikali kuu iliunga mkono ujenzi huo mwaka 2023 hadi utakapokamilika.