Tahadhari matumizi ya vyakula vyenye kemikali
4 September 2024, 13:10
Jamii imeshauriwa kutumia vyakula vya asili kuliko matumiz ya vyakula vyenye kemikali vivyozaliwa viwandani.
Na Hagai Ruyagila- Kasulu
Wazazi na walezi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kutumia vyakula vya asili ili kuwapatia watoto wao kwa ajili ya kuimalisha kinga zao za mwili kuliko kutumia vyakula vya viwandani ambavyo si salama kwa mtoto na mama mjamzito.
Wito huo umetolewa na Afisa afya na mratibu wa usalama wa vyakula halmashauri ya mji Kasulu Gilbert Moshi ambapo amesema ni vizuri kuepuka kumpa mtoto na mama mjamzito vyakula vya viwandani ili kuepuka magonjwa mbali mbali yasiyo ya kuambukizwa ikiwemo shinikizo la damu.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya ufuatiliaji na utekelezaji pamoja na itifaki (SMAUJATA) mkoa wa Kigoma Steven Kuyanga amesema mzazi anapompa mtoto chakula cha asili ambacho haki kemikali kitamsaidia mtoto kukukua katika afya njema.
Baadhi ya Wazazi na walezi kutoka halmashauri ya mji Kasulu wamesema kuna umuhimu mkubwa kwa mtoto kupewa chakula cha asili kwasababu kinavirutubisho vingi tofauti na chakula kilichopita kiwandani.