Jamii yatakiwa kuwalea watoto katika madili mema
2 September 2024, 13:00
Askofu mkuu wa Kanisa la Evangelical Methodist Church Tanzania (EMCT) lililopo kata ya Murusi wilayani Kasulu mkoani Kigoma Ngeze Mzimya ameitaka jamii kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kujenga taifa lenye ustawi bora kwa vizazi vijavyo na kiuchumi kwa ujumla.
Askofu Ngeze ametoa wito huo wakati akizungumza na radio joy fm baada ya ibada takatifu kanisani hapo
Amesema endapo watoto watalelewa katika maadili mema itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapata viongozi bora ambao wataweza kujenga uchumi imara wa taifa hili la Tanzania.
Aidha Askofu Ngeze amesema wazazi kutowalea watoto wao katika maadili mema imesababisha watoto kuiga utamaduni kutoka nchi ya nje hali inayopelekea kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii.
Kwa upande wake Abiudi Bihunira Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo amesema jamii inatakiwa kuwa na upendo ambao hauna unafiki ndani yake ili kuenenda katika maadili mema ambayo yasaidia katika ndoa, familia na jamii kwa ujumla.
Nao wazazi kutoka wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamesema malezi bora ndiyo chachu ya maendeleo katika taifa lolote ulimwenguni.