Joy FM

NGO’s zatakiwa kuwekeza miradi inayogusa wananchi

22 August 2024, 13:48

Katibu tawala wa mkoa wa kigoma akizungumza katika kongamano la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Picha na Lucas Hoha

Serikali ya mkoa wa kigoma imeyataka mashirika yanayofanya kazi mkoani kigoma kuwekeza zaidi kwenye miradi itakayosaidia wananchi.

Na Lucas Hoha – Kigoma

Mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyopo mkoa wa kigoma yametakiwa kuwekeza kwenye miradi inayogusa maisha ya wananchi ikiwemo maji, afya na afua za lishe kwa kuzingatia miongozo, kanuni na Sheria za nchi.

Wito huo umetolewa na katibu tawala wa mkoa wa kigoma Hassan Rugwa ambaye alikuwa  mgeni rasmi kwenye jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa kigoma social Hall uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Amesema mashirika hayo yana mchango mkubwa katika kuwaleta wananchi wa kigoma maendeleo  wakishirikiana na serikali.

Kwa upande wake, mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali Alex Isack amesema wataendelea kuzingatia maelekezo ya serikali katika kuleta maendeleo ikiwemo kuwekeza kwenye miradi inayoleta tija kwa wananchi

Mwakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali akizungumza wakati wa kikao cha mashirika, Picha na Lucas Hoha

Nao baadhi ya wadau walioshiriki jukwaa hilo wakiwemo Maafisa maendeleo ya jamii wamesema mashirika yasiyo ya serikali ni nguzo ya kukuza uchumi wa nchi na kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika hayo ili yaweze kufanya kazi kwa ufanisi

Katika jukwaa hilo mashirika yasiyo ya kiserikali yametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sukari kwa watoto wenye mahitaji maalumu waliopo kituo Cha kulea watoto yatima matyazo na watoto wa shule maalumu ya Uvinza.