Waziri wa Uvuvi azindua kiwanda cha kuchakata mazao ya uvuvi
16 August 2024, 15:00
Serikali imesema kuwa itaendelea kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wa ndani na nje ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki.
Na Lucas Hoha – Kigoma
Waziri wa mifugo na Uvuvi nchini Abdallah Ulega amewahakikishia wananchi wa mkoa wa kigoma kuwa serikali imedhamiria kwa dhati kuufungua mkoa huo kuwa lango la biashara katika sekta mhimu ikiwemo kujenga viwanda vya uvuvi ili wananchi kujikwamua kiuchumi.
Mh. Ulega ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi ikiwemo kiwanda Cha Mkuyu Fish Export kilichopo kata ya kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Amesema ujenzi wa viwanda hivyo itasaidia vijana kupata ajira.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa kigoma Kamishina jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli amesema uongozi wa mkoa wa kigoma utatoa ushirikiano kwa wawekezaji huku akitaja baadhi ya mambo mhimu ambayo yamefanywa na serikali ikiwemo kujenga barabara, uboreshaji wa uwanja wa ndege na uboreshwaji wa hospitali.
Kwa upande wao baadhi wa viongozi ambao wamewekeza viwanda vya uchakataji wa mazao ya Uvuvi wameomba serikali kupunguza Kodi na kulinda rasilimali za ziwa Tanganyika Ili samaki wapatikane muda wote.