Joy FM

Vijiji 2 vyapatiwa hati miliki za kimila 500 Kigoma

16 August 2024, 12:30

Wananchi wa vijiji vya Mwamgongo na Kigalye wakiwa na hati miliki za kimila,Picha Jacob Ruvilo

Wananchi 500 wa vijiji vya Mwamgongo na Kigalye katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma wameanza kunufaika na mpango wa awamu ya pili kupatiwa bure  hati miliki za kimila ambazo tayari zimekamilika kati ya hati miliki za kimila 4272 zilizopangwa kutolewa kwa vijiji vitano chini ya taasisi ya Jane Goodall Tanzania tangu mwaka 2023.

Mwanahabari wetu Jacob Ruvilo amehudhuria hafla ya ugawaji wa hatimiliki hizo na kutuandalia ripoti ifuatayo