Ziwa Tanganyika kufunguliwa rasmi Agosti 15
14 August 2024, 13:58
Serikali iliamua kuchukua uamzi wa kufunga Ziwa Tanganyika na shughuli za uvuvi ili kupisha mazalia ya samaki kuongezeka kutokana na kwamba uvuvi haramu umekuwa ukiathiri ukuaji wa samaki ambao wanavuliwa kiharamu.
Na Lucas Hoha – Kigoma
Wakati shughuli za uvuvi zikiwa zinaelekea kufunguliwa katika ziwa Tanganyika, Mkurugenzi wa Uvuvi nchini Prof. Mohammed Shekhe amewaagiza wavuvi kutumia kanuni na sheria za uvuvi ili kuepuka uharibifu wa mazalia ya samaki kwa mara nyingine.
Doria maalum ya ukaguzi ndani ya Ziwa Tanganyika iliyofanywa na mkurugenzi wa uvuvi nchini pamoja na viongozi wengine akiwemo mhifadhi wa Ziwa Tanganyika Agnely Lishela zikiwa zimesalia siku mbili tu shughuli za uvuvi kuanza upya.
Mkugenzi huyo amewatoa hofu wananchi na wavuvi kuwa serikali ilifunga ziwa hilo kwa nia njema nakuwa hawatarajii kuona wavuvi wanakiuka kanuni na sheria za uvuvi.
Kwa upande wake Mhifadhi wa Ziwa Tanganyika Agnely Lishela amesema, katika kipindi ambacho shuguri za uvuvi zilikuwa zimefungwa hakuna wavuvi ambao wamekamatwa wakivua kihole, huku akiwatoa hofu wananchi wa mkoa wa kigoma kuwa serikali haijaongeza siku za kulifunga ziwa hilo.
Shughuri za uvuvi katika Ziwa Tanganyika zilifungwa kwa muda wa miezi 3 tangu may 15 mwaka wa 2024 kwa lengo la kuacha samaki kuzaliana na kuongeza mazao yatokanayo uvuvi ndani ya ziwa hilo na sasa linafunguliwa Augost 15 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa mifungo na uvuvi Abdallah Alega.