Wadau watakiwa kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu
7 August 2024, 12:04
Serikali wilayani kasulu mkoani kigoma imewataka wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ili kuhakisha wanafunzi wanapata elimu bora.
Na Emmanuel Kamangu – Kasulu
Wadau wa maendeleo wilayani Kasulu wameaswa kuendelea kumuunga mkono Raisi Dkatari samia suruhu hasani katika kuhakikisha shule za msingi zinakuwa na miundombinu ya kutosha ya Tehama ili kuongeza ufaulu mashuleni.
Ameeleza hayo mdau wa maendeleo Bw, Ezra Mikamba wakati akikabidhi komputa mbili moja kwa shule ya msingi nyankole na nyingine kwa shule ya msingi titye zote zikiwa ni shule za kata ya titye na lengo ikiwa ni kuwasaidia walimu kuchapa mitihiani ya mazoezi shuleni na kuondokana na garama za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za stationari
Kwa upande wake Mratibu Elimu kata ya titye Bw, Yoabu Hinyula amewaomba walimu kutumia komputa hizo kutoa majaribio ya kutosha kwa wanafunzi jambo litakalo saidia kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa.
Aidha mwalimu wa Talumu shule ya msingi titye Bw. Gabriel Magarya pamoja na mkuu wa shule ya msingi nyankole Bw,Jaktan Nyakimwe kwa pamoja wamemshukuru Bw, Mikamba kwa msaada huo kwani utasaidia kuondokana na adha ya kuchapisha mitihani nje na shule zao.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi titye na nyankole mmoja wao akiwa Malaki Leonadi wamesema komputa hizo ni nyenzo bora ya kusoma kwa vitendo somo la tehema na kuongeza ufaulu katika somo hilo.