Joy FM

Wafanyabiashara walia na utitiri wa kodi Kigoma

1 August 2024, 08:54

Baadhi ya wafanyabiashara kigoma wakiwa na viongozi mbalimbali katika kikao cha baraza la biashara, Picha na Lucas Hoha

Serikali ya mkoa Kigoma imesema itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ii waweze kufanyabiashara kwa urahisi kwa kuweka mindombinu bora ya usafiri na usafirishaji.

Na Lucas Hoha – Kigoma

Wafanyabiashara Mkoani Kigoma wameomba Serikali kupunguza utitili wa Kodi zinazotozwa mipakani hasa katika bandari za mkoa wa kigoma na kuboresha miundombinu yakufanyia biashara kwa kujenga masoko ya kisasa, reli ya kisasa SGR na barabara ili kufanya biashara katika mazingira rafiki.

Wafanyabiashara hao wametoa maoni hayo wakati wa kikao cha baraza la biashara mkoa wa kigoma na kuwa uwepo wa vikwazo vya Kodi na miundombinu isiyo rafiki inasababisha watu kushindwa kufanya kwa uhuru na kupata faida.

Mkuu wa mkoa kigoma Thobias Andengenye akiwa na viongozi wa mkoa pamoja na wafanyabiashara, Picha na ucas Hoha

“Nadhani njia bora ya kuondoa kodi ambazo zimekuwa zikiwaminya wafanyabiashara ni pamoja na serikali kuja na mpango wa ulipaji koda kwa mamlaka moja na sio mamaka zinazotoza kodi kuwa zaidi ya moja kwa wakati tofauti tofauti”

Sauti ya wafanyabiashara mkoa wa kigoma

Akijibu hoj hizo,  Mkuu wa mkoa wa kigoma Kamishna jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji   Thobias  Andengenye amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 11 ili kuboresha miundombinu ya biashara ikiwemo kujenga reli ya kisasa, kuboresha bandari za ziwa Tanganyika huku akitoa msimamo wa serikali katika kupunguza utitili wa Kodi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye
Mkuu wa mkoa kigoma Mh. Thobias Andengenye akizungumza wakati wa baraza a biashara mkoa wa kigoma, Picha na ucas Hoha
Sauti ya wadau wa kodi kigoma

Nao baadhi ya viongozi wanaliohudhuria baraza hilo la biashara wakiwemo Mamlaka ya mapato tanzania mkoa wa kigoma wamesema watasimamia vema masuala ya Kodi kwa kuzingatia Sheria zilizowekwa na serikali na kuhakikisha mifumo ukusanyaji wa Kodi inasomana.