Joy FM

Wananchi kuachana na matumizi ya kuni kutunza mazingira

1 August 2024, 09:45

Wananchi wakiapanda miti ili kulinda mazingira, Picha na Mtandao

Hamashauri ya wilaya Kigoma imesema itaendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti ili kulinda mazingira kwa manufaa ya baadaye.

Na Orida Sayon – Kigoma Dc

Wananchi Wilayani Kigoma wametakiwa kutunza mazingira kwa kupanda miti ili  kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayokabili maeneo mbalimbali ya nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu tawala wilaya ya kigoma Bw. Mganwa Nzota  akizungumza na Joy FM katika  zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo ilipojengwa nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambapo jumla ya miti 120 imepandwa kati ya miti 500 inayotarajiwa kupandwa katika eneo hilo.

Amesema  zoezi  hilo lina lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluh Hassan katika kampeni ya utunzaji mazingira ili yaweze kusaidia katika uendelevu wa viumbe hai. 

Katibu tawala wilaya ya kigoma Bw. Mganwa Nzota

Kwa upande wake,  Mkuu wa Idara ya Maliasili na uhifadhi wa mazingira  Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw.Vicent  Mhezi ameeleza faida za upandaji na uwepo wa miti katika mazingira yanayomzunguka binadamu na kueleza namna gani idara inashirikisha jamii kuhakikisha inatunza mazingira.

Bw.Vicent  Mhezi

Hata hivyo licha ya wananchi kupewa elimu ya utunzaji mazingira na faida za kupanda miti bado wanaendelea kuwa mabalozi  katika  jamii  zao katika ajenda nzima ya kupanda miti ili kulinda mazingira .

wananchi