Joy FM

Usafi wa mazingira pasua kichwa Kasulu mji

26 July 2024, 10:02

Afisa afya mazingira ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha udhibiti wa taka halmashauri ya Mji Kasulu Bw.Msafiri Charles, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali katika halmashauri ya mji wa kasulu mkoani kigoma imesema inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wanadhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kuwachukulia hatua za kisheria wanaochafua mazingira.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wadau wa maendeleo katika halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha suala la usafi na utunzaji wa mazingira ili wananchi waweze kuona umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Kuelekea siku ya usafi wa mazingira julai 27 mwaka huu Afisa afya mazingira ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha udhibiti wa taka halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Msafiri Charles amesema baadhi ya wadau wa maendeleo wamelipa kisogo suala la usafi na utunzaji wa mazingira. 

Amesema katika siku hiyo wamejipanga kuwashirikisha wadau hao kuona umuhimu wa kutunza mazingira na kufanya usafi kwa kuwa wanayo nafasi kubwa ya kuweka kipaumbele kwenye suala la usafi katika shughuli wanazozifanya.

Sauti ya Afisa afya mazingira halmashauri ya Mji Kasulu Bw.Msafiri Charles

Aidha Bw.Charles amesema lengo wa kuwashirikisha wadau hao wa maendeleo ni kwa sababu bajeti ya serikali inakuwa na mambo mengi hivyo uwepo wao utasaidia kuiweka wilaya ya Kasulu katika hali nzuri.

Sauti ya Afisa afya mazingira halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Msafiri Charles

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa maendeleo wilayani Kasulu wamesema wanatambua umuhimu wa kutunza mazingira huku wakionyesha utayari wao wa kushirikiana na serikali katika suala hilo.

Sauti ya wadau wa maendeleo mjini Kasulu