Joy FM

Mwenyekiti atuhumiwa kuiba na vifaa vya ujenzi

18 July 2024, 08:17

Wananchi buhigwe wakiwa kwenye mkutano wa hadhara, Picha na Mtandao

Mkuu wa wilaya Buhogwe Michael Ngayalina amemwagiza afisa utumishi kumtafuta mwenyekiti wa kijiji cha songambele ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili ikiwemo wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule hali iliyosababisha ujenzi kusimama.

Na Michael Ngayalina – Buhigwe

Wananchi wa kijiji cha songambele kata ya mnyegera wilayani Buhigwe mkoani kigoma amemuomba Mkuu wa wilaya hiyo kumuagiza mwenyekiti wa kijiji hicho kurejesha vifaa vya ujenzi alivyochukua na kupelekea kushindwa kuendelea na ujaenzi wa shule ya sekondari katika kijiji hicho

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha songambele Bw. Julias Ntagata emeibua hoja hiyo mbele ya mkuu wa wilaya ya buhigwe kanali Michael Ngayalina katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi ambapo ameomba vifaa vya ujenzi vilivyochukuliwa na mwenyekiti wa kijiji hicho virejeshwe kwakuwa vilikwamisha ujenzi wa shule ya sekondari kijijini hapo.

Sauti ya mwananchi akitoa malalamiko ya mwenyekiti kuiba vifaa vya ujenzi

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael ngayalina akahitaji kupata maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji hicho kuhusu malalamiko ya wananchi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael ngayalina
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael ngayalina, Picha na Mtandao

Aidha amemuagiza Afisa utumishi katika halmashauri ya wilaya ya Buhigwe kuitisha kikao na serikali ya kijiji ili kumhoji mweyekiti kuwa ni lini atarejesha vifaa hivyo pamoja na kutoa maelezo baadhi ya malalamiko kuhusu uuzwaji wa viwanja kinyume cha sheria.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael ngayalina