Wananchi mtumie fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi
16 July 2024, 16:13
Inaelezwa kuwa uwepo wa fursa mbalimbali za kiuchumi katika halmashauri ya mji wa kasulu mkoani kigpma wananchi wameshauriwa kutumia fursa hizo kwa ajili kujiongezea kipato na kuinua uchumi wao na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Wananchi Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamewatakiwa kutumia fursa zinazowazunguka ili kufanikisha malengo yao waliyojiwekea katika maisha yao.
Hayo yamebainishwa na mchungaji Father Canon Kalebu Zephania Subdean msaidizi wa askofu kanisa kuu la Mtakatifu Andrea Dayosisi ya Western Tanganyika wakati wa ibada ya kuzindua kanda ya Kasulu Mjini katika kanisa la Kristo Mfalme anglikana Murusi Mjini Kasulu Mkoani Kigoma.
Amesema usipojifahamu huwezi kujua fursa zilizopo katika jamii inazokuzunguka ambazo zitakusaidia kufanikisha malengo yao.
Aidha mchungaji father Canon Kalebu amesema huwezi kukata tamaa njia ya kufanikiwa ni kuthubutu ili kuzishinda changamoto zilizopo katika maisha yako nakutumia vizuri fursa zilizopo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu wamesema watazitumia fursa zilizopo kwa kuongeza kipato ili waweze kufanikiwa katika maisha yao.