Joy FM

Bilioni 2 zaboresha miundombinu ya elimu

16 July 2024, 11:30

Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Prof.Joyce ndalichako

Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali imeendelea kutenga pesa kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule ili kuchochea kiwango cha ufaulu kwa wananchi kwa kuwa na mazingira bora na rafiki kwa kujifunza.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Serikali katika halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma imeendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari ili kutatua changamoto inayozikabili ya shule hizo.

Akizungumza na wananchi, waalimu pamoja na wanafunzi wa shule za msingi Murusi na Kasulu Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Prof.Joyce ndalichako amesema Zaidi ya billion 2 zilizotolewa na serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 zimetumika katika kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari.

Prof.Ndalichako amesema bado serikali inaendelea na ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Prof.Joyce ndalichako

Aidha Kulingana na prof.ndalichako anasema licha ya jitihada za ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari katika kata ya murusi bado mrundikano wa wanafunzi ni mkubwa kwa baadhi ya shule ambapo  serikali imekamilisha ujenzi wa shule sekondari kidyama ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Prof.Joyce ndalichako

Baadhi wananchi mjini Kasulu wameipongeza serikali kwa kutatua changamoto ya madawati jambo ambalo litasaidia wanafunzi kufanya vizuri kitaaluma.

Sauti ya Wananchi mjini kasulu