Dkt. Mpango amkalia kooni mkandarasi anayejenga barabara ya Buhigwe -Kasulu
10 July 2024, 16:00
Wizara ya ujenzi kupitia kwa waziri wake Innocent Bashungwa ametakiwa kuhakikisha kumsimamia mkandarasi anajenga barabara ya Buhigwe hdi Kasulu ili iweze kukamilika kwa wakati.
Na Josephine Kiravu – Buhigwe
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amemtaka Mkandarasi anayejenga barabara ya Kasulu- Buhigwe, Manyovu kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ifikapo Machi 2025 kwani Kukamilika kwa Barabara hiyo ambayo ni sehemu ya ujenzi wa bararaba ya Kabingo-Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa Km.260.6
Akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Buhigwe, Mhe. Dkt. Mpango amesema maendeleo ya mkoa yamechelewa kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu bora ya barabara, umeme na huduma nyingine za kijamii hivyo wananchi mkoani hapa wanapaswa kutumia fursa ya kukamilika kwa huduma hizo kujiimarisha kimaendeleo.
Upande wake Waziri wa Ujenzi Inocent Bashungwa amemuhakikishia Makamu wa Rais kuwa barabara ya Kasulu Manyovu itakamilika ifikapo Machi 2025 ili kuruhusu wananchi kuitumia na kuondokana na adha wanazozipata kutokana na kutokamilika kwa barabara hiyo.
Aidha katika hatua nyingine akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya usambazaji wa Nishati ya Umeme wilayani Buhigwe, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema jumla ya vijiji 107 havina umeme, ambapo vijiji 97 mkandarasi yupo kazini na vingine 14 vipo katika hatua ya kufanyiwa Tathmini.
Amesema Wizara kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamefanikiwa kuvifikia vijiji vyote wilayani humo japo utekelezaji wa kazi ya kuweka umeme hufanyika kwa awamu kuendana na Bajeti inavyopangwa na serikali.