Dkt. Mpango aelekeza barabara ya Malagarasi -Uvinza kukamilika kwa wakati
9 July 2024, 09:04
Serikali imesema inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo barabara na umeme ili kuhakikisha mkoa wa kigoma unafunguka na kuwa kitovu cha biashara kutokana na kupakana na nchi za Congo na Burundi.
Na Josephine Kiravu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Philip Isdor Mpango amemtaka waziri wa Ujenzi kuhakikisha anamsimamia mkandarasi anaetekeleza ujenzi wa barabara ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza anakamilisha kwa wakati.
Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo akiwa ziarani wilayani uvinza Mkoani Kigoma ambapo ameanza ziara yake kwa kufanya ukaguzi wa maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo mbapo amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutasaidia kufungua mkoa wa kigoma na mikoa mingine lakini na nchi jirani ikiwemo Burundi na Congo.
“tumetembea kwenye vumbi kwa muda mrefu sana nikuombe waziri wa ujenzi simamia ujenzi wa barabara hiii ikamilike ili wananchi wasipate usumbufu kwenye kusafirisha bidhaa zao dhamira ya rais ni kuona wananchi wanapata huduma bora”
Na hapa Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa anaeleza hatua zilizofikiwa na matarajio ya kukamilika kwa mradi huo wa barabara.
Hata hivyo mbali na kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Makamu wa Rais amezungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Uvinza pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye kituo Cha kupoza umeme katika eneo la Kidahwe.
Makamu wa Rais ataendelea na ziara yake ya kikazi kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege Kigoma.