Joy FM

Wananchi walalamikia michango mingi shuleni

4 July 2024, 12:02

Wananfunzi wa shule ya msingi wakiwa katika kongamano

Wazazi na walezi wilayani kibondo Mkoani Kigoma wametakiwa wameomba serikali kupunguza baadhi ya michango midogo midogo ambayo hutozwa shuleni kutokana na hali kuwa ngumu ya maisha.

Na James Jovin – Kibondo

Wakati shule tayari zimefunguliwa kwa muhula wa pili kwa msimu wa masomo mwaka 2024 wazazi na walezi wametakiwa kutambua majukumu yao kwa wanafunzi lakini pia kuelewa  huduma zinazotolewa na serikali ikiwemo elimu bila malipo.

Hatua hiyo imekuja katika Mkutano wa Hadhala uliofanyika Kata ya Kibondo Mjini ambapo baadhi ya wazazi wamelalamikia michango wanayotozwa mashuleni ikiwemo chakula cha mchana na fedha za kulipa walinzi licha ya uwezo wa kifedha kwa baadhi ya wazazi na walezi kuwa mdogo

Mmoja wa wananchi waliohudhulia mkutano huo wa hadhara bwana Marko Emili amewataka diwani wa kata ya kibondo mjini pamoja na mbunge wa jimbo la muhambwe kushughulikia changamoto hizo ili kuwasaidia majukumu wazazi wasio na kipato na hivyo wanafunzi kuhudhulia masomo bila wasi wasi.

Sauti ya Mmoja wa wananchi waliohudhulia mkutano huo wa hadhara bwana Marko Emili

  Kwa upande wake diwani wa kata ya Kibondo mjini bw. Alex Baragomwa amewataka Wazazi na walezi kuacha tabia ya kukwepa majukumu yao kwani maelekezo ya elimu bila Malipo yanaeleweka na kwamba serikali imekuwa ikifanya majukumu makubwa ya kujenga miundombinu hivyo wazazi pia wanao wajibu wa kuandaa baadhi ya mahitaji ya wanafunzi na si kuachia serikali mzigo wote.

Naye mbunge wa jimbo la muhambwe dr. Frolence Samizi ameishukuru serikali kwa kazi kubwa iliyofanya ya kuandaa miundo mbinu hali asilimia kubwa ya shule za sekondari na msingi kuwa na miundo mbinu ya kutosha kwa wanafunzi wote hivyo kuboresha elimu na kukuza taaluma kwa wanafunzi.