Joy FM

Meneja TRA mbaroni, kukutwa na meno ya tembo Kibondo

4 July 2024, 09:55

Ni Mwa TRA Kibondo baada ya kukamatwa na nyara za serikali, Picha na mtandao

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma kigoma limesema litaendelea kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na uhabifu wa nyara za serikali ili kuwa fundisho kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Na Kadislaus Ezekiel – Kigoma

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma, limethibitisha kumkamata meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA wilayani Kibondo Bwana Irving Mutegeki, kwa tuhuma za kukutwa na nyara za Serikali ikiwemo meno ya tembo mawili, kwenye gari yenye namba ya usajili STL 7274 aina ya toyota landcruiser ikiwa na namba ya usajili bandia T.501 AGS. 

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Iddi Kiyogomo amesema mtuhumiwa amekamatwa kufuatia ukaguzi wa magari na abiria katika kizuizi cha polisi barabara ya kibondo- kakonko eneo la kihomoko akiwa anasafiri kuelekea mkoa wa kagera.

Sauti ya Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Iddi Kiyogomo

Wananchi mkoani Kigoma, wameomba hatua zichukuliwe halaka ikiwemo kufikishwa mahakamani kutoa fundisho kwa viongozi wengine.

Sauti ya Wananchi mkoani Kigoma