Zaidi ya shule 9 Uvinza zina uhaba wa madawati 1,000
2 July 2024, 15:57
Wananchi wa kata ya Ilagala wilayani Uvinza mkoani Kigoma wameomba serikali kuwasaidia kupunguza tatizo la madawati linazozikubwa shule za kata hiyo ili kuwasaidia watoto kuondokana na tatizola kukaa chini
Na Kadislaus Ezekiel – Uvinza
Shule za msingi zaidi ya tisa katika kata ya Ilagala wilayani Uvinza mkoani Kigoma, zinakabiliwa na uhaba wa madawati zaidi ya elfu moja, hali inayosababisha wanafunzi wengi kusoma wakiwa wamekaa chini na kuwa kikwazo katika ujifunzaji na ufundishaji.
Baadhi ya wazazi wakizungumzia suala la ukosefu wa madawati, wakati wa uzinduzi wa kukabidhi madawati miatatu, kwa shule za msingi za kata ya Ilagala, ambazo zimetolewa na mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ilagala na mdau wa maendeleo thadeo ndenzako wameomba serikali na wadau wengine kusaidia upatikanaji wa madawati ya kutosha.
Mdau wa maendeleo Thadeo Ndenzako amesema atakabidhi madawati miatatu kwa shule zote za kata ya ilagala ili kusaidia watoto kuepuka kukaa chini wakiwa shule.
Kaimu mratibu elimu kata, kata ya ilagala jonathan mayane amesema shule zote za kata zinaupungufu wa madawati zaidi ya elfu moja ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi, wakati mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinnah Mathamani, katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Chama Cha Mapindu mkoa wa Kigoma Sarah Kairanya amesema atahakikisha saula hilo linafanyiwa kazi mara chini ya Tamisemi ili kusaidia wananafunzi.